Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ina jumla ya Idara (13) na Vitengo sita (6). Kuna Tarafa nne (4), Kata ishirini na nane (28), Vijiji mia moja na moja (101)
Idara ya Utumishi ndio Idara MAMA katika Halmashauri kwani Masuala yote ya Kiutumishi yanafanyika katika Idara hii
Kimsingi Idara ya Utumishi na Utawala katika kutekeleza majumu yake inazingatia misingi ya Utawala BORA katika kutoa huduma bora kwa Watumishi na Jamii kwa ujumla.
Majukumu ya Idara:-
Kuandaa bajeti ya mishahara na ikama ya watumishi.
Kutafsiri na kushughulikia miundo ya Utumishi.
Kuajiri kwa kuomba vibali vya ajira Utumishi Makao Makuu.
Kupandisha vyeo na kuthibitisha watumishi kazini.
Kusimamia na kushughulikia maadili na nidhamu za watumishi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo.
Kusimamia na kuhakikisha vikao na mikutano yote ya kisheri na kikanuni Katika ngazi zote inafanyika.
Kuandaa na kusimamia mpango wa mafunzo kwa watumishi wakiwa nje na ndani ya vituo vya kazi.
Kushughulikia mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi, Waheshimiwa Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.
Kutathimini utendaji kazi wa watumishi.
Kushughulikia mambo ya itifaki kwa watumishi.
Kufanya ukaguzi wa Payroll ya mishahara kwa kwa kushirikiana na wakuu wa Idara kila mwezi na kutolea taarifa iwapo kutakuwa na mapungufu au usahihi wa payroll husika.
Kuhakikisha watumishi wote ambao muda wao umefikia ukomo kwa sababu mbali mbali wanaondolewa katika payroll kupitia Mfumo wa LAWSON.
Kuandaa Tange kwa kila robo ya mwaka na mwaka mzima.
Kutafsiri sheria, kanuni na nyaraka mbali mbali za Serikali katika utumishi wa umma.
Kutekeleza miongozo na mazoezi ya kitaifa yanayo tolewa.
Kusimamia ulinzi na usalama wa mali zote za Halmashauri.
Kushughulikia haki na stahiki za watumishi .
Kusimamia Mifumo ya usafiri wa magari ya Halmashauri.
Kushirikiana na Taasisi zingine katika masuala mbalimbali ya kiutendaji