Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson, ameshukuru na kupongeza ujio wa mgeni rasmi pamoja na wadau waliotoa msaada kwa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko, akisema kuwa msaada huo ni faraja kubwa kwa shule hiyo inayotoa huduma za ziada kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Wilaya ya Ikungi.

Akizungumza hayo leo tar 03 Januari 2026 katika ukumbi wa Shule hiyo, wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida, Mhe. Apson amesema shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko ina wanafunzi wakiwemo watoto wenye mahitaji maalum, na imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuwafundisha na kuwasaidia watoto hao ili waweze kupata elimu kwa usawa.
Katika tukio hilo, mahitaji mbalimbali yametolewa ikiwemo kalamu, madaftari na sabuni zoezi lilihusisha pia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kama sehemu ya mchango wao katika kuimarisha elimu na ustawi wa watoto wenye mahitaji maalum.

Mhe. Apson ameishukuru na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa mchango wake endelevu katika kuiunga mkono shule hiyo, hususan katika masuala ya huduma za kijamii na elimu jumuishi.

Katika tukio naye Mgeni Rasmi, Mhe. Zubeir Ali Maulid amewaunga mkono UWT kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 3 kwa ajili ya kusaidia mahitaji mbalimbali katika shule hiyo.

Shughuli hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), yanayolenga kuendeleza mshikamano wa kijamii na kuwajali makundi maalum katika jamii.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa