SERIKALI Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na wananchi mapema leo asubuhi wameupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Manispaa ya Singida ambapo
Furaha tupu eneo la makabidhiano.
SERIKALI Wilayani Ikungi Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na wananchi mapema leo asubuhi wameupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Manispaa ya Singida ambapo utazindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Sh. 2.9 Bilioni
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mwenge huo na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri katika Kijiji cha Utaho, Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro alisema Mwenge utakimbizwa kilometa 92.5 na kukagua miradi ya maendeleo.
Alisema Mwenge huo utaanza mbio zake kwa kutembelea Shule ya Msingi Samamba kukagua madarasa na mindombinu iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kuzindua klabu ya rushwa na kupanda miti.
Alitaja baadhi ya miradi mingine itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru kuwa ni Mradi wa ufyatuaji wa Matofali wa Kikundi cha Jitume Vijana, Mradi wa TEHAMA Sekondari ya Ikungi, Kuweka jiwe la msingi la Kituo cha Mafuta cha JMC, kukagua mifumo ya huduma ya afya Kituo cha afya Ikungi na kuzindua vyumba vya maabara za Sayansi Shule ya Sekondari ya Unyahati.
Muro alitumia nafasi hiyo kuwatambulisha viongozi mbalimbali waliokuwepo kuupokea Mwenge wa Uhuru akiwepo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Winfrida Funto ambaye alikuwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wajumbe wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti, Wabunge, Wananchi, Viongozi wa dini, Watumishi wa Halmashauri hiyo Madiwani na wanafunzi

Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa