Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi Ndg Justice Kijazi amegawa pikipiki mpya 8 kwa watendaji wa kata katika majimbo mawili wilaya ya Ikungi kwa ajili ya shughuli za kiserikali hasa ukusanyaji wa mapato kwenye kata zao...Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo kwa watendaji tarehe 20 Februari 2023 Kijazi amesema kuwa pikipiki hizo zitumike kukusanya mapato na sio shughuli zingine tofauti na maelekezo hayo...Pikipiki nane zimekabidhiwa kwenye kata 8 zilizopo majimbo mawili Ikungi magharibi ni Kata ya Iyumbu,Ighombwe,Iglansoni na Mwaru lakini Ikungi Mashariki ni kata ya Issuna,Mang'onyi,Ntuntu Pamoja na Misughaa.Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally J. Mwanga amewataka watendaji kutunza pikipiki hizo ili ziweze kudumu na kusaidia katika matumizi ya kiserikali.Piki piki hizo zimetolewa na TAMISEMI na kupokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Jijini Dodoma.Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi20/02/2023.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa