• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Ikungi District Council
Ikungi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Tekolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Utawala
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbailmbali
    • Fomu Malimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Vituo vya habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya picha
  • Takwimu za Wilaya
    • Sensa 2022
      • Matokeo ngazi ya Taifa na Mkoa
      • Matokeo ngazi ya wilaya na kata
      • Matokeo ngazi ya vijiji
      • Kasi ya ongezeko la watu
      • Idadi ya kaya
      • Idadi ya watu kwa umri
      • Matokeo ngazi ya tarafa
    • Takwimu za Elimu
      • Orodha ya Shule kwa kata
      • Idadi ya wanafunzi
        • Msingi
        • Sekondari
    • Nyanja ya Afya
      • Idadi ya vituo vya afya kwa kata
      • Afya nyinginezo
    • Ikungi yetu
    • Takwimu za miradi

WANANCHI WAPEWE TAARIFA ZA MADINI - BITEKO

Posted on: November 20th, 2018


 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuhakikisha unatoa taarifa za tafiti zake zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ili wachimbaji wadogo waweze kuzitumia katika kubaini madini yaliyopo na kuanza kuchimba kwa kufuata sheria na kanuni za madini.Naibu Waziri Biteko alitoa agizo hilo tarehe 19 Novemba 2018 kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi wilayani Ikungi mkoani Singida kama sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wa madini.Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira bora ya uchimbaji  wa madini kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa mbalimbali  za utafiti zilizofanywa na Wakala wa Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na kampuni za utafiti wa madini lengo  likiwa  ni  kuhakikisha kuwa uchimbaji wao unakuwa wa uhakika na sio wa kubahatisha.Akielezea maboresho mengine yaliyofanywa katika sekta ya madini, Biteko alisema Serikali imeboresha  Sheria ya Madini inayotambua madini kama mali ya watanzania  yanayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 

Dkt. John Pombe Magufuli.Aliendelea kusema kuwa, Serikali imeweka mkakati wa kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini wasio rasmi na kuwapatia  leseni za madini ili uchimbaji wao ulete tija kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuunda vikundi na kupewa leseni ili waanze kuchimba na kulipa kodi Serikalini.“Sisi kama Serikali kupitia Wizara ya Madini lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaweka mazingira bora kwa wachimbaji wadogo wa madini ili uchimbaji uongeze kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia kodi na tozo mbalimbali,” alisema Biteko.Wakati huohuo Biteko aliwataka wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Shanta kutokuharibu miundombinu ya maji iliyowekwa ili iweze kunufaisha wananchi wote.Awali wakiwasilisha kero mbalimbali wakazi hao waliiomba Wizara ya Madini kuwapatia maeneo kwa ajili ya uchimbaji wa madini ili waweze kujiingizia kipato na kulipa kodi Serikalini.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo wa madini katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida, Consolata Joseph alisema kuwa uchimbaji wao  umekuwa ni wa kubahatisha na hata kuvamia maeneo yenye leseni kubwa ya madini inayomilikiwa na Kampuni ya Dhahabu ya Shanta.Awali akizungumza katika ziara hiyo, Meneja Mkuu  wa Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo wilayani Ikungi mkoani Singida, Philbert Rweyemamu alisema mgodi umeshaanza kutoa fidia na kuongeza kuwa mpaka sasa umeshatoa shilingi bilioni 2.6 pamoja na ujenzi wa makazi mbadala ambapo mpaka sasa wameshajenga nyumba sita.Aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu, mgodi unatarajia kukamilisha ujenzi wa nyumba nyingine sita na kufanya idadi ya nyumba kuwa 12 kama sehemu ya kuhakikisha wananchi wanaolipwa fidia wanaishi katika mazingira mazuri.Akizungumzia changamoto za mgodi wake, Rweyemamu alieleza kuwa ni pamoja na wachimbaji wadogo haramu kuvamia eneo la mgodi  na kuchimba madini, miundombinu kuhujumiwa na baadhi ya wananchi kugomea fidia inayotolewa na kampuni hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu akizungumza.Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiangalia makubaliano ya maandishi yaliyofanywa kati ya mmiliki wa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya General Business and Equipment Supply Limited.Uchimbaji wa madini ya jasi ukiendelea katika eneo la kampuni ya General Business and Equipment Supply Limited iliyopo katika eneo la Bumbua wilayani Itigi mkoani Singida

kwa hisani ya Afisa habari Singida

Matangazo

  • MPYA! MPYA! MPYA! TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPT 06, 2023 August 31, 2023
  • View All

Habari mpya

  • Elimu ya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yahitajika Ikungi

    April 17, 2025
  • Kamati ya Siasa Yapongeza Ujenzi wa Miradi Ikungi

    April 09, 2025
  • "Wanaume Hudumieni Wake Zenu" DC Apson Ikungi

    March 04, 2025
  • NEST yarahisisha manunuzi

    March 04, 2025
  • View All

Video

DC Muro atembelea Kata ya Mkiwa na kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mkiwa. Kazi inaendelea...
More Videos

Viunganishi vya haraka

Tovuti unganifu

  • EGA website
  • public service management
  • TAMISEMI website
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

    Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania

    Simu ya mezani: +255262964037/6

    Mobile:

    Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa