• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Ikungi District Council
Ikungi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Tekolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Utawala
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbailmbali
    • Fomu Malimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Vituo vya habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya picha
  • Takwimu za Wilaya
    • Sensa 2022
      • Matokeo ngazi ya Taifa na Mkoa
      • Matokeo ngazi ya wilaya na kata
      • Matokeo ngazi ya vijiji
      • Kasi ya ongezeko la watu
      • Idadi ya kaya
      • Idadi ya watu kwa umri
      • Matokeo ngazi ya tarafa
    • Takwimu za Elimu
      • Orodha ya Shule kwa kata
      • Idadi ya wanafunzi
        • Msingi
        • Sekondari
    • Nyanja ya Afya
      • Idadi ya vituo vya afya kwa kata
      • Afya nyinginezo
    • Ikungi yetu
    • Takwimu za miradi

97% ya watoto wanaozaliwa hunyonyeshwa maziwa ya mama.

Posted on: August 1st, 2022


Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Mwanaidi Khamis wakati akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kwa watoto kitaifa yanayofanyika kwenye halmashauri ya Ikungi Mkoani Singida.

Mhe. Mwanaidi ameendelea kusema kuwa 43% tu ya watoto  ndio hunyonyeshwa hadi kipindi cha miaka miwili na kuendelea huku takwimu zikionesha 57% tu ya watoto ndiyo hunyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kuchanganya na chakula kingine wala maji ndani ya kipindi cha miezi 6.

"Tafiti zinaeleza kuwa mtoto akizaliwa na kuanza kunyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja kunaweza kuokoa uhai wake kwani kuchelewa kumnyonyesha mtoto kuna changia kwa kiwango kikubwa vifo vya watoto wachanga ndani ya siku 28." Aliongeza.

Aidha, amesema hapa nchini unyonyeshaji wa watoto wachanga ndani ya saa moja umefikia 90% hivi sasa ikilinganishwa na 54% iliyokuwa mwaka 2018 wakati utoaji wa Vitamini A kwa watoto wa miezi 6-59 nao umeongezeka kutoka 64% mwaka 2018 hadi kufikia 97% hivi sasa.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwahimiza wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoa huduma kwa wakati husika na kuwaasa wazazi kuendelea kuhudhuria Kliniki kama inavyoagizwa pia wazazi kuwanyonyesha watoto wachanga maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita bila kumlisha chochote.

"Kunyonyesha maziwa ya mama kuna faida nyingi kwa mama na mtoto kwa kuwa kunaimarisha afya na ustawi wa mama na mtoto, vilevile unyonyeshaji watoto maziwa ya mama huzuia aina zote za utapiamlo kwa vile kuna kuwa na uhakika wa chakula kwa watoto wachanga na wadogo". Alisisitiza

Vile vile amesema ili kuimarisha na kuendeleza juhudi za kulinda Afya ya watoto kupitia unyonyeshaji maziwa ya mama, Serikali itaendelea kufuatilia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo iliyopo juu ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama, kuendelea kutenga fedha za kutekeleza afua za kuboresha ulishaji wa watoto ikiwemo elimu ya Afya, lishe na huduma za msingi kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na kutoa miongozo na taarifa sahihi kuhusu unyonyeshaji na namna ya kujikinga na magonjwa hasa ya mlipuko.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro amewataka wakurugenzi na watoa huduma ya Afya wa halmashauri yake kuendelea kutoa elimu juu ya unyonyeshaji na kuwasihi wananchi kuepukana na mimba za utotoni.

"Changamoto zinazopelekea wazazi kutonyonyesha watoto zao ni pamoja na mimba za utotoni kwakuwa hawajui umuhimu wa kunyonyesha na wengine kuwa bize na kazi na hivyo kuacha kunyonyesha watoto zao." Amesema DC Muro

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ametoa rai kwa Serikali kuongeza muda wa ruhusa kwa wazazi wanaofanya kazi ili kupata muda mwingi wa kuwanyonyesha watoto wao.

Maadhimisho hayo ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kwa watoto kitaifa yanayofanyika kwenye halmashauri ya Ikungi Mkoani Singida kuanzia 1-7 Augusti 2022 yenye kauli mbiu isemayo CHUKUA HATUA ENDELEZA UNYONYESHAJI: ELIMISHA NA TOA MSAADA

Matangazo

  • MPYA! MPYA! MPYA! TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPT 06, 2023 August 31, 2023
  • View All

Habari mpya

  • Msigala Aagiza kutungwa kwa Sheria Ndogo Kudhibiti chumvi

    May 09, 2025
  • Ikungi Kinara wa Miradi Bora

    May 08, 2025
  • Elimu ya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yahitajika Ikungi

    April 17, 2025
  • Kamati ya Siasa Yapongeza Ujenzi wa Miradi Ikungi

    April 09, 2025
  • View All

Video

DC Muro atembelea Kata ya Mkiwa na kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mkiwa. Kazi inaendelea...
More Videos

Viunganishi vya haraka

Tovuti unganifu

  • EGA website
  • public service management
  • TAMISEMI website
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

    Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania

    Simu ya mezani: +255262964037/6

    Mobile:

    Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa