Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice L. Kijazi,Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndg Jerry Murro pamoja na watoa mafunzo kutoka halmashauri hiyo wamezungumza na vikundi mbalimbali vya wanufaika wa mikopo juu ya umuhimu wa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati...
Akizungumza na wanavikundi hao Mkurugenzi Kijazi leo tarehe 21 septemba katika kata ya Unyahati amesema kuwa wanufaika wa mkopo warejeshe mikopo hiyo kwa wakati ili wengine waweze kukopa na kuepusha usumbufu usio walazima...
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndg Jerry Murro ameongeza na kusema kuwa familia zishirikiane na wanufaika wa mikopo ili kuzalisha fedha zitakazo wasaidia wote kwa pamoja kujikwamua kiuchumi."kina baba ishini vizuri na na familia zenu na kusirikiana katika shughuli za biashara ndogo ndogo ili mpate faida kubwa kupitia mikopo hiyo.''
Awali watoa mafuzo wakifundisha walisema kuwa mwanachama anapaswakujisajili na kupata ushauri wa namna ya kuendesha miradi yake hatimaye kurejesha mikopo hiyo kwa wakati...
Aidha mikopo hiyo hutolewa kwa kina mama, vijana pamoja na wote wenye ulemavu lengo ikiwa ni kukuza maendeleo ya jamii nzima kwa ujumla na kuondokana na lindi la umasikini...
Pia Kijazi aliwaomba wananchi wa unyahati kupima viwanja vyao kuelekea maandalizi ya ujenzi stendi,pamoja na kuwapa maeneo wawekezaji lengo ikiwa ni kupanga miji na kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia stendi na wawekezaji hao...
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa