Idara ya Mifugo na Uvuvi ni moja kati ya Idara 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Shughuli za idara ni pamoja na; kutoa huduma za Afya za mifugo, shughuli hii ina sehemu zifuatazo; Kinga, matibabu, udhibiti wa usafirishaji wa mifugo. Ushauri na mafunzo, Uzalishaji wa mifugo, Usalama wa mazao ya chakula yatokanayo na mifugo, Biashara ya mifugo, kusimamia uvuvi na ufugaji wa viumbe majini.
Lengo la shughuli hizi ni kwaajili ya kuboresha uzalishaji wa mifugo na kuinua mchango wa sekta ya mifugo na uvuvi kwenye pato la Taifa.
Msukumo ni kuongeza uzalishaji na ubora kuliko wingi wa mifugo kwa eneo. Kufanya ufugaji kuwa wa kibiashara, unaozalisha zaidi, endelevu, unaoongeza ajira na kulinda mazingira. Kuhamasisha, kulinda na kusimamia shughuli za ufugaji na uvuvi wa samaki, kusimamia biashara ya samaki kwa nia ya kuongeza lishe kwa jamii na mapato ya taifa.
WATAALAM
Idara inatakiwa kuwa na wataalam kwa ngazi ya Wilaya na ngazi za chini ( Kata na Vijiji) kama ifuatavyo ;
Ngazi ya Wilaya
Mtaalam wa viumbe vya majini (Uvuvi)
Mtaalam wa ugani
Mtaalam wa nyama na ngozi
Mtaalam wa Nyanda za malisho
Mtaalam wa wanyama wadodo
Mtaalam wa Utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo
Mtaalam wa sekta ya Maziwa
Daktari wa mifugo.
Ngazi za chini
Kila kata inatakiwa kuwa na mtaalam moja mwenye stashahada
Kila kijiji kinatakiwa kuwa na mtaalam moja mwenye astashahada.
MIFUGO NA MIUNDOMBINU
Mifugo.
Eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ni kubwa linafaa kwa kufuga mifugo ifuatayo kwa madhumuni mbalimbali;
Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, kuku, bata, sungura kwa idadi mbalimbali.
Kwa sasa aina na idadi ya mifugo iliyopo ni kama ifuatavyo;
Aina
|
Ng’ombe |
Mbuzi |
Kondoo |
Nguruwe |
Kuku |
Punda |
Mbwa |
Paka |
Idadi
|
554,800
|
244,400
|
145,012
|
802
|
395,200
|
4,201
|
17,205
|
3,255
|
Lengo la kufuga mifugo hii ni pamoja na Chakula, biashara (chanzo cha mapato) na wanyamakazi. Pia kuna mifugo rafiki kama mbwa na paka.
Miundombinu na maeneo ya malisho.
Maeneo ya malisho yaliyopo ni yale yaliyopo kwenye maeneo yasiyo na matumizi mengine, yanaweza kuvamiwa wakati wowote. Inashauriwa maeneo yaainishwe, yatengwe na kupimwa kwa ustawi wa sekta ya mifugo.
Aina
|
Majosho
|
Minanda (maeneo tu)
|
Vituo vya mifugo
|
Maduka ya pembejeo
|
Masoko ya kuku
|
Vituo vya utotoleshaji kuku
|
Idadi
|
35 |
4 |
4 |
8 |
3 |
2
|
Kutokana na uhaba wa vyanzo vya maji kama vile mito,maziwa na mabwawa pamoja na nvua chache katika halmashauri kazi za uvuvi zimekuwa kwa kiwango kidogo hivyo kuchangia kipato kidogo katika uchumi wa halmashauri, maeneo muhimu ya uzalishaji wa samaki ni ziwa Wembere lililopo kata za Mgungira na Iyumbu,ziwa Kimbwi lililopo kata Mungaa na Makiungu ,bwawa la Itigi lililopo katika kata ya Irisya na mabwawa ya watu binafsi katika kata za Ikungi na Ihanja .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa