Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndugu. Kastori Msigala aagiza kulipwa kwa stahiki za watumishi kadri fedha zinapokuja ili kupunguza changamoto hiyo kuboresha ufanisi katika utendaji kazi.
Hayo yamesemwa hii leo Tarehe 01 Octoba, 2025 katika kata ya Dung'unyi na Siuyu alipokuwa akitembelea miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi wa kata hizo
Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa kuna haja ya kupitia na kubaini stahiki za watumishi mbalimbali ili kujua changamoto zao na kuzitatua kwa wakati lengo ni kuongeza ufanisi kazini.
Baadhi ya watumishi wameeleza changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa fedha za uhamisho na likizo, kupanda madaraja na changamoto za mfumo wa PEPMIS kwani wengi wao wanaishi katika mazingira yasiyokuwa na mtandao wakutosha ili kujaza na kutuma kazi zao kwa wakati.
Sambamba na hilo Mkurugenzi Msigala ametembelea ujenzi wa madarasa matatu na matundu sita ya vyoo shule ya msingi Samaka kwa gharama ya milioni 79.2, ukamilishaji wa matundu manne ya vyoo zahanati ya Samaka kwa gharama ya milioni mbili, ujenziwa matundu nane ya vyoo shule ya msingi Damankiya mradi huo unagharimu milioni 13.6 na kuagiza kukamilika kwa miradi hiyo mapema ili kutoa huduma kwa wananchi.
Hata hivyo Mkurugenzi ameagiza kupelekwa milioni 23 kukamilisha madarasa matatu shule ya msingi Kipumbwiko, milioni 15 ukamilishaji wa zahanati ya Samaka, milioni 13 ukamilishaji vyoo damankia shule ya msingi, milioni 10 ujenzi wa matundu 14 ya vyoo shule ya sekondari Siuyu, milioni 10 shule ya msingi unyakanya kudhibiti upungufu wa madawati, pamoja na milioni 10 ujenzi wa vyoo shule ya msingi Nali
“Changamoto ya upungufu wa nyumba za watumishi tunaweka kwenye bajeti ijayo ikiwa ni pamoja na kuongeza watumishi mbalimbali kadri serikali ya Jamhri ya Muungano wa Tanzania itakavyotuletea watumishi wapya” amezungumza Msigala
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa