Idara ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Idara 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Shughuli za Idara
Kuelimisha jamii zitambue kuwa rasilimali za kuleta maendeleo ziko ndani ya jamii zenyewe na kwamba wanao uwezo wa kuzibaini na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo yao badala ya kusubiri serikali au wadau wengine wa Maendeleo.
Kuhakikisha kuwa mipango na shughuli zote zinazofanywa na jamii ziwe zenye kuleta maendeleo yenye kuzingatia jinsia.
Kuhamasisha na kutambua vikundi vya wanawake wajasiriamali na kutoa mafunzo/ elimu ya ujasiriamali.
Idara inatoa mikopo kwa wanawake kupitia vikundi vya watu watano.
Idara inatoa elimu ya ujasiriamali na ubunifu mbalimbali kwa vikundi vya vijana.
Idara inaratibu shughuli za maendeleo ya vijana na kuwapatia mikopo.
Idara inatoa elimu ya stadi za maisha na afya ya uzazi kwa vijana.
Kutembelea na kuvitambua vituo vya kulelea watoto pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wasimamizi wa vituo hivyo.
Kujenga uelewa kwa jamii kuhusu masuala ya jinsia na maendeleo kupitia wataalamu wa Idara.
Utambuzi wa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kushirikiana na asasi mbalimbali.
Kutoa mikopo kwa wanawake na vijana na kuwapatia mafunzo juu ya mbinu za kuendesha biashara na kuzingatia masharti ya mikopo bila itikadi wala siasa.
Kutoa elimu ya lishe bora kwa watoto wadogo na malezi yanayostahili na kupiga vita ajira ya watoto.
Kuhamasisha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali zenye kutoa maamuzi ili jamii itambue uwezo wa wanawake.
Kufanya ufatiliaji wa mara kwa mara kwa vikundi vya uzalishaji mali vya vijana na wanawake.
Kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya kuweka na kukopa kwa kushirikiana na Idara ya Ushirika.
Kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kuleta maendeleo na usawa wa kijinsia.
Idara inaratibu shughuli zinazoendeshwa na Mashirika ya hiyari katika Halmashauri kwa kutoa ushauri na miongozo ya namna ya kuendesha shughuli zao pamoja na kuwaunganisha na wadau wengine wa maendeleo.