Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi yatoa mafunzo ya mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote ambao unamhakikishia kila mwananchi kupata huduma bora za afya bila kikwazo cha gharama anapohitaji huduma hizo.

Mafunzo hayo yametolewa tarehe 09 Januari, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo waganga wafawidhi, watendaji wa kata na Vijiji pamoja na wataalamu mbalimbali wa afya wameshiriki ili kufahamu faidi za mfumo huo kwa manufaa ya wananchi wote.
Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo Katibu Tawala wilaya ya Ikungi Mhe. Rashid M. Rashid akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson amesema kuwa Mpango huu ni utekelezaji wa sera ya Serikali ya awamu ya sita inayolenga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya kwa wakati kwa gharama nafuu na kwa usawa bila kujali hali zao za kiuchumi.
Hata hivyo, Sheria hii inatarajia kuanza kutekelezwa kwa majaribio kwa baadhi ya makundi maalum yasiyokuwa na uwezo yakiwemo wazee wenye miaka 60 na kuendelea, watoto chini ya miaka 5, wanawake wajawazito na watu wenye ulemavu, kuanzia januari 2026 na hasa wale wanaopata uwezeshwaji kutoka TASAF
"Hii ni katika kutekeleza ahadi ya Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa ya kuanzisha Bima ya afya kwa wote ndani ya siku 100" amezungumza Rashid
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa