Kitengo cha TEHAMA ni moja ya vitengo sita (6) katika Halmashauri ya Ikungi. Kitengo hiki kina watumishi wawili ambao ni:
Amour Omary Eljabry
Eva Gaitani Myula
Kitengo hiki kinafanya kazi ya kusimamia matumizi sahihi na salama ya vifaa vya TEHAMA na Kusimamia Mifumo yote inayotumika katika Halmashauri ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.
UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MBALI MBALI
Kitengo hiki kinafanya shughuli zifuatazo:
i. Kuhakikisha mifumo yote inayotumika katika Halmashauri inafanya kazi kwa ufanisi. Mifumo hiyo ni :-
Mfumo wa kukusanyia Mapato (LGRCIS),
Mfumo wa matumizi ya fedha zote za Halmashauri (EPICOR),
Mfumo wa kuandaa bajeti ya Halmashauri (PLANREP),
Mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa katika vituo vya kutolea huduma (FFARS),
Mfumo wa kutolea takwimu za Elimu Msingi na Sekondari (BEMIS),
Mfumo wa kusimamia mishahara ya watumishi na utunzaji wa taarifa za watumishi (LAWSON),
Mfumo wa usajili wa wanafunzi wa Elimu Msingi (PREM),
Mfumo wa utunzaji taarifa za walengwa (PSSN) ,
Mfumo wa kutolea taarifa za wagonjwa (GoT- HoMIS),
Mfumo wa kutolea taarifa za usimamizi wa shule (SIS) ambao umeanza kutumika kwa ngazi ya Elimu Msingi na
Mfumo wa kutolea vibali vya kusafiria nje ya nchi ambao unapatikana kwa kiunganishi cha https://safari.gov.go.tz
Kurekebisha miundo mbinu ya mtandao wa ndani (LAN) pale inapotokea hitilafu ya mawasiliano
Kusimamia tovuti ya Halmashauri ambayo inapatikana kwa kiunganishi cha www.ikungidc.go.tz
Kuhakikisha POS za kukusanyia mapato zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa na taarifa zote za ukusanyaji zinatumwa kwenye server kuu iliyopo TAMISEMI
Kutoa Elimu kwa watendaji kuhusu utumiaji wa mashine za POS
Kutembelea vituo vya afya na kutatua changamoto zinazojitokeza katika mfumo wa kutolea taarifa za wagonjwa (GoT- HoMIS) na kufanya kazi zingine tunazopangiwa na Mkurugenzi.