Afisa Tehama Bi- Eva Myula akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi aitaka kamati ya mpango wa taifa wa Kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA kata ya Dung'unyi kuzingatia wanayofundishwa ili kwenda kuokoa jamii inayopitia matatizo ya Ukatili mbalimbali.Bi-Myula amesema kuwa huo ni mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili nchini dhidi ya wanawake na watoto hivyo baada ya mafuzo hayo anategemea kuona visa vingi dhidi ya ukatili vikiripotiwa na kufanyiwa kazi kupitia vyombo vyetu vya Afya na Sheria.Afisa Tehama Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya Siku mbili ya Tarehe 14 na 15 Septemba 2023 katika Ukumbi wa sekondari ya Unyahati ambapo alisisitiza usiri katika utekelezaji wa Mpango huo kwani matukio mengi ya ukatili hulenga kuharibu saikolojia za watendwa hivyo mhusika anaporipoti anategemea kuona yupo salama kwa kila namna.Aidha kwa upande wake Bi-Mariam Mwandikile amesema kuwa mpango huo umeanzishwa mwaka 2017/2018 na kuanza utekelezaji wake mwaka 2021/2022 ambapo wanalenga kuzifikia kata 10 katika Wilaya ya Ikungi ambazo ni Puma,Ihanja,Kituntu,Makiungu,Mungaa,Lighwa,Sepuka,Mtunduru,Issuna na Dung'unyi."Kila tunapotoa mafunzo huwa tunaandaa mpango kazi wa jinsi ya kupunguza matukio ya ukatili na hatimaye kuyamaliza kabisa katika Wilaya ya Ikungi"Alisema Afisa Maendeleo ya Jamii Ikungi Mwandikile Mafunzo hayo ya siku mbili yanawezeshwa na Mdau wa Maendeleo Social Action Trust Fund SATF ambao ni wawezeshaji mahususi wa kamati ya MTAKUWWA Wilayani Hapa ambapo makao makuu yake ni Dar es Salaam wakishirikiana na OVCT ambayo makao makuu yake ni Puma.Shirika hilo linawezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kaya masikini kiuchumi ili watoto hao waweze kufikia ndoto zao.Mwisho Afisa Maendeleo Mwandikile ameongeza na kusema kuwa kuna madhara mbalimbali yatajitokeza ikiwa tutaruhusu ukatili kuendelea,na madhara hayo ni pamoja na kuongezeka kwa vifo,magonjwa,athari za kisaikolojia,umasikini,migogoro na kadhalika hivyo hatuna budi kutokomeza ukatili Ikungi.MWISHOAfisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi14/09/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa