Baraza la Madiwani Wilaya ya Ikungi lapitisha Bajeti ya Bilioni 39,025,760,000 kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024,na TARURA ni Bilioni 4,472,543,784.47 pamoja na RUWASA ni Bilioni 2,312,872,728.61...
Awali Bajeti hiyo imepitiwa na kujadiliwa (CMT) timu ya menejimenti halmashauri,kamati ya Fedha pamoja na kamati ya ushauri Wilaya ili kujiridhisha na rasimu ya mpango wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024...
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba alikua mgeni rasmi katika Baraza hilo la Madiwani ambalo lilifanyika tarehe 16 Februari,2023 katika ukumbi wa halmashauri huku akisisitiza Madiwani kufatilia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ili ikamilike wa wakati na kwa ubora unaohitajika."naomba muwe mabalozi wazuri kwa wananchi wenu kusemea mazuri yanayofayika na serikali ya Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan"alisema Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Kwa upande wao Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi
Ndg Justice Kijazi pamoja na Mwenyeki wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe Ally J.Mwanga wameahidi kusimamia miradi kadri Bajeti ilivyopangwa kuhakikisha maendeleo yanakua kwa Kasi wilayani Ikungi.
Aidha Mkuu wa Wilaya mpya Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amesema anatarajia kuwa na ziara ya kukagua miradi mbalimbali aliyokabidhiwa na Mhe Jerry Muro Mkuu wa Wilaya Mstaafu ili kuiendeleza na kuanzisha mipya kadri Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 itakavyoruhusu.
MWISHO
AFISA HABARI
HALMASHAURI WILAYA IKUNGI
TAREHE 16, FEBRUARI 2023Baraza la Madiwani Wilaya ya Ikungi lapitisha Bajeti ya Bilioni 39,025,760,000 kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024,na TARURA ni Bilioni 4,472,543,784.47 pamoja na RUWASA ni Bilioni 2,312,872,728.61...
Awali Bajeti hiyo imepitiwa na kujadiliwa (CMT) timu ya menejimenti halmashauri,kamati ya Fedha pamoja na kamati ya ushauri Wilaya ili kujiridhisha na rasimu ya mpango wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024...
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba alikua mgeni rasmi katika Baraza hilo la Madiwani ambalo lilifanyika tarehe 16 Februari,2023 katika ukumbi wa halmashauri huku akisisitiza Madiwani kufatilia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ili ikamilike wa wakati na kwa ubora unaohitajika."naomba muwe mabalozi wazuri kwa wananchi wenu kusemea mazuri yanayofayika na serikali ya Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan"alisema Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Kwa upande wao Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi
Ndg Justice Kijazi pamoja na Mwenyeki wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe Ally J.Mwanga wameahidi kusimamia miradi kadri Bajeti ilivyopangwa kuhakikisha maendeleo yanakua kwa Kasi wilayani Ikungi.
Aidha Mkuu wa Wilaya mpya Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amesema anatarajia kuwa na ziara ya kukagua miradi mbalimbali aliyokabidhiwa na Mhe Jerry Muro Mkuu wa Wilaya Mstaafu ili kuiendeleza na kuanzisha mipya kadri Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 itakavyoruhusu.
MWISHO
AFISA HABARI
HALMASHAURI WILAYA IKUNGI
TAREHE 16, FEBRUARI 2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa