Baraza la madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi laridhia kuipokea kampuni ya SOLDECOM AGRO L.T.D kampuni zawa ya kitanzania inayojihusisha na shughuli
mbalimbali za kibiashara ikiwemo biashara ya hewa ya ukaa hapa Tanzania na nchi
nyingine pia.
Akizungumza katika baraza hilo hii leo tarehe 06 Februari, 2025 Mwenyekiti wq Halmshauri Mhe. Ally J. Mwanga amesema kuwa Ikungi ilipata nafasi ya mafunzo ya uzalishaji ya hewa ya ukaa kupitia Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika kutokana na uwepo wa misitu katika Wilaya ya Ikungi sawa na Tanganyika na inauwezo wakuzalisha hewa hiyo ili kiwe chanzo cha mapato.
"Hivyo tumeridhia kwa moyo wote kupata wawekezaji hawa wa SOLDECOM AGRO LTD ili hewa ya ukaa iweze kuzalishwa katika Wilaya ya Ikungi hususani msitu wa Minyughe na Baadae wakiridhia msitu wa Mlilii" amesema mwenyekiti wa Halmshauri Mhe Ally J.Mwanga
Akiwasilisha taarifa katika baraza hilo mratibu wa hewa ya ukaa Bwana Barakael Solomon amesema kuwa Kupitia mradi wa kuhifadhi msitu wa Minyughe tutaweza kupunguza madhara yatokanayo
na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanatokana na ongezeko la joto duniani.
Mratibu huyo ameongeza na kusema kuwa tunakwenda kupanda miti palipokatwa miti hasa maeneo ya pembezoni
mwa msitu pia kuulinda msitu usivamiwe na kuharibiwa na watu ili
uweze kujizalisha upya.
Kampuni hii imesajiliwa kisheria kupitia BRELA na pia imeshasajiliwa na
taasisi ya kudhibiti na kuratibu shughuli za biashara ya hewa ya ukaa yenye makao yake
makuu mkoani Morogoro yaani National Carbon Monitoring Centre (NCMC) ambayo ndio inayotoa mwongozo wa namna biashara ya hewa ya ukaa inavyofanyika nchini.
Hata hivyo baraza limejadili taarifa za mapato na matumizi na kuhimiza juu ya ukusanyanyi wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato kwani mapato ya Halmshauri ndio chanzo cha maendeleo ya wananchi Wilayani hapa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa