Divisheni ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na divisheni ya elimu sekondari na msingi inaendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na elimu ya ukatili dhidi ya watoto.
Elimu hiyo imekuwa ikitolewa pia katika jamii kupitia mikutano ya hadhara inayofayika katika kata mbalimbali wilayani Ikungi
Akisoma taarifa ya utekelezaji shughuli mbalimbali za kudhibiti UKIMWI na virusi vya UKIMWI kwa kipindi cha cha Januari - Machi 2025 katika kamati ya UKIMWI Afisa maendeleo ya jamii amesema kuwa kwa kushirikiana na divisheni ya afya wamekuwa wakisambaza condom jumla ya pisi 33,600 katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanajikinga na maambukizi hayo.
"Pia kumekuwa na uundaji wa klabu za mapambano dhidi ya ukimwi mashuleni ili kutoa elimu kwa wanafunzi na adhari za ugonjwa huo katika jamii"amezungumza Afisa maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe. Ally J. Mwanga amesema changamoto zilizopo ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa maendeleo ya jamii katika baadhi ya maeneo ambao ni waratibu wa UKIMWI ngazi ya jamii hali inayopelekea kutokupata elimu na msaada pale unapohitajika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa