Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi leo tarehe 16 mei 2024,wametembelewa na wageni kutoka Wizara ya Elimu na Tamisemi kwa udhamini wa shirika la Campain for Female Education(CAMFED ) kwa lengo la kutoa elimu ya Stadi za maisha . Katika ziara hiyo wageni hao wamesema wamekuja kutoa mafunzo ya elimu ya stadi za maisha kwa vijana wa elimu ya sekondari kidato cha kwanza na pili lengo elimu hii imwandae kijana kimaisha . Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amewashukuru wadau hao na kuwaomba kuja mara kwa mara na kwa upendeleo zaidi ili wilaya ya Ikungi ipate vijana wengi zaidi wenye elimu ya stadi za maisha. Mwisho wadau hao wamesema walishatoa elimu hiyo tayari kwa Halmashauri 35 ikiwemo Mkoa wa Singida walitoa elimu hiyo kwa Halmashauri mbili tu,kwa sasa wamesema wataongeza halmashauri zote tano zilizobaki kwa Mkoa wa Singida na kufikia Halmshauri 41 kwa nchi nzima.Wameongeza kwa kusema watatoa mafunzo kwa wakuu wa shule za serikali na Maafisa elimu kata ili waende kuwaelimisha Vijana.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa