Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson atoa maagizo kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Kwa Maafisa Elimu Kata na Watendaji wa Kata na Vijiji juu ya kuwasisitiza wazazi kuandikisha watoto wao kuanza masomo na usambazaji wa Mbegu za Ruzuku katika Vijiji vyote Wilayani hapa.Hayo yamesemwa Leo Tarehe 18 Januari,2024 alipokuwa akizungumza na Watendaji wa kata,Vijiji pamoja na Maafisa Elimu Kata kuwa Zaidi ya Bilioni 1.4 zimetolewa Kwa ajili ya ujenzi wa madarasa lengo ni watoto wote wapate Elimu katika mazingira rafiki hivyo ni jukumu letu kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule."Ni agizo kuwa Viongozi wapite nyumba kwa nyumba ili watoto wote waende shule,Kuna tabia ya wazazi kuwatumia watoto katika kilimo hali inayopelekea watoto kuchelewa kuanza masomo na wengine kutowapeleka kabisa, wazazi wa namna hii wachukuliwe hatua za kisheria".Wakisoma taarifa ya hali ya Uandikishaji wa Wanafunzi Afisa Elimu Sekondari Ndg Ngwano J.Ngwano pamoja na Afisa Elimu Msingi na Awali Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Margaret Kapolesya wanesema Kwa upande wa Uandikishaji kidato Cha kwanza umefikiwa Kwa asilimia 63.5 na upande wa Elimu ya Awali ni asilimia 67 Darasa la kwanza ni asilimia 70 Na Bado wanasisitiza viongozi kushirikiana Kwa karibu na wananchi kuhakikisha Wanafunzi wote wanaandikishwa mapema."Na Kuna wengine wanaandikishwa baadae wanakuwa watoro na ndoa za utotoni tushirikiane kudhibiti hilo"Amesema Bi Kapolesya.Hata hivyo Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amesisitiza kuongezeka Kwa kasi ya usambazaji wa Mbegu zinazotolewa Kwa bei ya Ruzuku ili wakulima waweze kulima Kwa wakati na kuongeza uchumi wa Wilaya yetuKikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Mwenyekiti na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambao wote wamesisitiza maagizo hayo kutekelezwa ipasavyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa