Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia majalada ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida akiwa katika zaira ya kikazi ya siku moja katika mkoa huo tarehe 11 Januari 2021.
Wa pili kulia ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Singida Shamim Hoza na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Ikungi Ambroce Ngonyani. Wa kwanza kulia ni Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi bi. Eva Myula
Hata hivyo, Waziri Lukuvi alisema Watendaji wa Mitaa na Vijiji watakaokasimia mamlaka ya usimamizi ardhi katika maeneo yao hawatakuwa na jukumu la kugawa, kupanga, kupima na kumilikisha ardhi bali kuangalia yanayoendelea katika mitaa yao na wakikuta ukiukwaji wowote kama vile ujenzi holela basi watakuwa na wajibu wa kusitisha.
” Kumbukumbu zote za masuala ya ardhi wajulishwe watendaji wa mitaa na vijiji ili waweze kufuatilia katika mitaa yao maana katika suala la hati za kimila tumefanya vizur ngazi ya vijiji ila suala la Hati Miliki za Ardhi bado tuko nyuma maana tumeficha taarifa wilayani” alisema Lukuvi.
Katika ziara yake Waziri wa Ardhi mbali na kutembelea halmashauri za wilaya ya Singida na Ikungi na kusisitiza kuwa halmashauri ndizo zenye jukumu la kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika maeneo yake na jukumu hilo siyo la maafisa ardhi.
Lukuvi alisema Halmashauri zote zijue zina wajibu wa kusimamia ardhi katika maeneo yao na ilichofanya Wizara ya Ardhi ni kuwapatia wataalam watakaowasaidia kujua namna bora ya kutumia ardhi vizuri.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa