Kamati ya huduma za mikopo katika Halmashauri ya wilaya ya Ikungi yatembelea vikundi mbali mbali vilivoomba mkopo wa asilimia 10 (10%) unaotolea kupitia mapato ya ndani ya halmashauri...
Zoezi hilo limefanyika likiwa na lengo la kudadisi na kuhakiki vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwamba wanakidhi vigezo vya kupewa mkoa na kurudisha kwa wakati sahihi...
Zaidi ya milioni 187 zinatarajiwa kutolewa na kamati hiyo mara baada ya vikao vya kisheria kukamilika...
Akizungumza na Mwandishi wetu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Bi Haika Massawe amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kukuza Ajira kuonge kipato kwa mwananchi na kuleta maendeleo katika wilaya ya Ikungi.
----------------------------------------------------
MWISHO
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
25/012023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa