Halmashauri ya ikungi imevuka lengo lilitorajiwa katika kampeni ya chanjo ya polio awamu ya tatu, kwa kutoa chanjo ya polio jumla ya ya watoto 97,575 sawa na asilimia 125.68.
akizungumza ofisini kwake na mwandishi wa habari hizi ,Mganga mkuu halmashauri ya ikungi , Dkt solomon Michael amethibitisha kuwa idadi ya watoto waliopatiwa chanjo ya polio wakati wa kampeni ya chanjo hiyo kwa awamu ya 3, imezidi makisio na kufikia asilimia 125.68.
Daktari Solomon Michael ametaja siri kubwa ya mafanikio ya kuvuka malengo ni kutoa elimu na hamasa kwa jamii juu ya umuhimu wa chanjo hiyo, pamoja na mikakati thabiti kwa kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii, iliyo wawezesha kutoa huduma hiyo nyumba kwa nyumba.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa