Katibu Tawala Mkoa wa Singida
Dkt. Fatma Mganga afanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali Wilaya ya Ikungi na kutoa maagizo juu ya ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora.
Ziara hiyo imeanza hii leo tarehe 08 Mei, 2025 katika mradi wa ujenzi wa mabweni mawili, madarasa manne pamoja na matundu 10 ya vyoo Shule ya sekondari Nkuhi Mtaturu unaogharimu milioni 454, mradi wa ujenzi wa vyumba 20 vya maduka stendi mpya ya Ikungi unaogharimu 172.5, mradi wa ujenzi wa njia za kutembea kwa miguu (walk ways) hospitali ya Wilaya ya Ikungi unaogharimu milioni 194.2 ,mradi wa ujenzi vyumba vya maduka 21 mgahawa na vyoo uliopo Manispaa ya Singida unaogharimu milioni 285.
Pia Katibu Tawala ametembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kintandaa unaogharimu takribani milioni 544.2 pamoja na mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na matundu 6 ya vyoo ambapo mradi unagharimu milioni 58.6.
Katibu Tawala wa mkoa amepongeza ubora wa miradi hiyo na wasimamizi wa wa miradi hiyo na amesisitiza ikamilike kwa wakati ili iweze kuleta manufaa kwa maslahi mapana ya wananchi.
"Miradi yote hiyo ipi hatua za ukamilishaji hivyo kuna umuhimu kuongezwa kwa mafundi ili kazi mbalimbali ziendelee kwa pamoja ili ifikapo tarehe 30 mwezi huu miradi yote iwe tayari" amezungumza Katibu Tawala Mkoa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg.Kastory Msigala amemalizia kwa kushukuru juu ya ujio wa Katibu tawala na kuendelea kutekeleza maagizo ya Katibu Tawala kwa lengo la kuboresha miradi hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa