Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 zilizinduliwa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tarehe 01 April, 2023 Mkoani Mtwara na zilihitimishwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tarehe 14 Oktoba, 2023 Mkoani Manyara, baada ya kukimbizwa katika Wilaya, Halmashauri za Wilaya zote 195 za Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa siku 195 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apason pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice L.Kijazi anawashukuru viongozi na wananchi wote Wilayani hapa kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru katika kufanikisha shughuli hii kubwa na muhimu kwa Taifa letu wakati wa Mbio hizo za mwenge Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi amesema Halmashauri za Miji, Wilaya, Manispaa na Majiji zilishindanishwa kuzingatia vigezo kuhusu ushiriki wake katika shughuli za Mwenge wa Uhuru hususani katika utekelezaji wa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 na usimamiaji wa shughuli mbalimbali za Maendeleo ya wananchi .“Hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuibuka washindi kimkoa mkoani Singida ikifuatiwa na Singida Manispaa nafasi ya pili,Manyoni nafasi ya tatu,Itigi nafasi ya nne,singida DC nafasi ya tano,Mkalama nafasi ya sita na Iramba ni nafasi ya 7.MWISHO Imetolewa na,Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi1/12/2023#mwenge#mwengewauhuru2023@daniel_godfrey_chongolo@baba_keagan@singidars @mkalamadc @manyonidc @itigi_dc @iramba_district @singidamc
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa