Kamati ya Lishe Wilaya ya Ikungi yajadili kuboreshwa kwa Shughuli za utengenezaji wa Chunvi na uwekaji wa Madini joto kwenye chuvi Kata ya Kikio kwani Kupitia uboreshaji huo Halmashauri itatengeneze mapato kukuza maendeleo ya Wilaya.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndg Justice L.Kijazi amesema kuwa Ofisi ya mipango iweke utaratibu ambao utasaidia swala hilo kuwekwa kwenye bajeti ijayo ili Kutengeneza miundombinu wezeshi ya utengenezaji wa chumvi bora kwa matumizi ya kawaida na biashara nje na ndani ya Ikungi.Aidha amewataka viongozi wa lishe kuweka utaratibu ambao utasaidia wataalamu kwenda kujifunza Wilaya ya Iramba au kwingineko ili kuja na mpango kazi utakaowezesha kuanza rasmi Uchimbaji wa Chumvi kibiashara na sio uchimbaji kiholela usiofata mbinu za kitaalamu lengo ikiwa ni kuongeza vyanzo vya mapato ya Halmashauri Ikungi.Afisa Lishe Nevu Dickson Wilaya ya Ikungi amesema amepokea kilichojadiliwa kamati hiyo na kuihakukishia kamati kushirikiana nayo kikamilifu ili kuimarisha sekta ya lishe Wilayani Ikungi.Kamati pia imepitia na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za Lishe Robo ya kwanza Julai hadi Septemba 2023/2024 na Idara hizo ni pamoja na Idara ya Afya,Idara ya Elimu awali Msingi na Sekondari,Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi,Idara ya Habari na Mawasiliano pamoja na Idara ya Maendeleo ya Jamii.MWISHO IMETOLEWA NA;AFISA HABARI (W)IKUNGI04/12/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa