Wilaya ya Ikungi yapokea Gari moja kati ya magari matatu yanayotarajiwa kuletwa katika Wilaya ya Ikungi ambayo yatatumika katika Divisheni ya Afya kumuwezesha Mganga Mkuu wa Wilaya na watumishi wenzake kuwafikia wananchi na watumishi wa Afya kwa urahisi tofauti na mwanzo.Akizungumza katika Hafla fupi ya makabidhiano ya Magari hayo Waziri wa wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa Mkoani Singida viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida amesema Magari hayo yakatumike kwa shughuli mahususi za sekta ya Afya."Waganga wakuu nendeni mkafikie vituo vya Afya vyote na zahanati vijijini kusikiliza kero zao na kutatua changamoto zao ili kutoa huduma bora kwa wananchi." Amesema Mchengerwa.Mganga mkuu Wilaya ya Ikungi Dkt Dorisila Mlenga kwa upande wake amesema ameweka mikakati mingi na yupo tayari kuwafikia watumishi wote Hospitali ya Wilaya vituo vya afya na zahanati zote kwa wakati kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi."Kufanya kazi kwa bidii ndio namna nzuri ya kusema asante kwa Mama yetu kipenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania ambaye ameamua kutatua changamoto ya usafiri kwa Wilaya yetu". Amezungumza Dkt DorisillaSambamba na hilo amesema atahakikisha kwa kushirikiana na Halmashauri kulitunza gari hilo ili liweze kudumu zaidi na kutatua kero nyingi zaidi za wananchi kwani hata hivyo Halmashauri ipo katika kipundi cha umaliziaji wa vituo vya Afya na zahanati kupitia mapato ya ndani hivyo ni rahisi kusimamia umaliziaji huo kwa karibu.Mara baada ya Hafla hiyo ya makabidhiano Mhe Waziri alitembelea Barabara ya Kiwango cha Lami Wilaya ya Ikungi na Shule mpya ya Msingi Mtaturu iliyopo Ikungi na kuridhishwa na Miradi hiyo."Kuna Wilaya zingine wameomba kuongezwa fedha za ujenzi ila Ikungi imemaliza ujenzi ndani ya Bajeti jambo ambali sio lakawaida mnahitaji pongezi kubwa na Wilaya zingine wajifunze kutoka kwenu"Alizungumza Waziri.MWISHOImetolewa na,Afisa HabariHalmashauri (W) ya Ikungi13/12/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa