Tarehe 10/12/2018 ilikuwa ni siku ya kufunga siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto. Sherehe hizo zilifanyika katiak ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi,
ambapo watoto wenye uhitaji wa mahitaji maalumu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko walishiriki.
TPF-NET SINGIDA Ilifanya maadhimisho hayo yakiwa na kauli mbiu USALAMA WAKE WAJIBU WANGU.
"Matendo ya ukatili wa kijinsia lazima yatokomezwe kutokana na ushirikiano wa jamii husika" Jeshi la polisi mkoani singida limekemea makosa ya jinai yanayosababisha ukatili wa kijinsia... alisema mgeni rasmi RPC SWEETBART NYEWIKE.
Ameitaka jamii kufichua matendo ya unyanyasaji wa kijinsia kupitia dawati maalumu ambapo kutakuwepo wa usiri wa taarifa.
naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ikungi ndugu Justice Kijazi katika hafla hiyo ameahidi kushughulikia changamoto wanazozipata wanafunzi wa mahitaji maalum.
Changamoto hizo zimesomwa na mkuu wa shule ya msingi Ikungi Mwl Loth Ntandu.
Ametaja changamoto hizo ni pamoja shida ya maji shuleni hapo pamoja na upungufu wa vitendea kazi kwa ajili ya mahitaji ya watoto wenye ulemavu
"Serikali ya awamu ya Tano inatambua changamoto za shule hii, na kila mwezi inatoa kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuchangia elimu. hii ni juhudi kubwa kwa wilaya yetu ya Ikungi''
aliendelea kusema kuna fedha ya washiriki wa maendeleo EQUIP- T nazo zinatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
kuhusu changamoto ya maji ndugu Kijazi amesema Halmashauri ya wilaya Ikungi tayari imeshasaini mikataba ya visima nane zitakazo gawanywa kwenye kata mbalimbali, hivo kupunguza changamoto ya maji shuleni hapo
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ikungi akipokea zawadi mbalimbali kwa ajili wa watoto wenye mahitaji maalumu
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Winfrida Funto
Washiriki waliofika kwenyemaadhimisho ya ukatili wa kijinsia
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa