Kamati ya fedha na Mipango yafanya ziara yake leo tarehe 21 Octoba, 2024 katika Stendi Mpya inayojengwa vibanda vya biashara kuzunguka eneo hilo ambapo ujenzi wake upo hatu ya msingi na mradi huo unatarajiwa kugharimu taribani milioni 187 ikiwa ni moja ya huduma kwa jamii CSR kutoka katika Mgodi wa Santa uliopo Mkoa wa Singida Wilayani Ikungi.
Lakini pia kamati hiyo imetembelea mradi mpya ambao halmashauri inahitaji kuanzisha wa ujenzi wa mgahawa wa kisasa pamoja na majengo ya biashara katika kiwanja kilichopo manispaa ya Singida na mradi huo upo hatua za usafishaji wa kiwanja na ujenzi huo utaanza hivi punde.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Ally J. Mwanga akizungumza na wanakamati mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa ipo haja ya miradi hiyo kukamilika kwa wakati kutokana na hali ya mvua inayoendelea lakini pia kwa ajili ya maslahi mapana ya halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuingiza mapato ya ndani kupitia vyanzo hivyo vipya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa