Umati wa watu wajazana kwenye banda la maonyesho la halmashauri ya wilaya ya Ikungi, leo tarehe 8/8/2022 katika kilele cha siku ya wakulima na wafugaji kwemye viwanja vya nane nane nzuguni dodoma.
Kaimu mkuu wa idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Ndugu Gurisha msemo akihojiwa na mwandishi wa habari hii alisema " halmashauri ya wilaya ya Ikungi mwaka huu imeshiriki maonyesho ya nane nane na kutoa wakulima 11 kushiriki maonyesho ya kanda ya kati, ambapo wataonyesha na kutangaza kilimo cha mazao ya kipaombele ya kitaifa ambacho ni kilimo cha alizeti na korosho. mazao haya yanalimwa kwa wingi na yanastawi vizuri wilayani kwetu hivyo tunawakaribisha wawekezaji kutumia fursa hiii ya kilimo cha alizeti na korosho"
aliendelea kwa kusema kupitia maonyesho haya tumeweza kutangaza maeneo makubwa ya uwekezaji yenye ukubwa wa ekari 11500 ambayo yana ekari 4500 ya alizeti na yanayobaki kwa kilimo cha korosho. watu wote mnakaribishwa ofisi za mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya ikungi kupewa taratibu za kupata maeneo ya uwekezaji.
Halmashauri ya wilaya ya ikungi imefanikiwa kumpata mshindi namba wa 1. kilimo cha umwagiliaji ndugu Kitundu Mkumbo ambaye analima hekari sita na kuweza kupata zaidi ya shilingi milioni kumi kwa Mwaka.
baadhi ya wananchi waliojitokeza kutembelea banda la maonyeso Ikungi
mzee Aloyce mkulima kutoka Puma akitoa maelezo ya uzalishaji wa zao la uwele na mtama katika banda la halmashauri ya wilaya ya Ikungi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa