Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amepokea Kilo 3000 sawa na tani 3 za mbegu ya Ufuta kutoka katika Kampuni ya Uchimbaji wa Madini inayotarajiwa kugawiwa bure katika vijiji vitano kata ya Mang'onyi kama vile Mlumbi,Tupendane,Mwau,Sambaru na Mang'onyi.Akizungumza na Wananchi Tarehe 12 Novemba 2023 Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kuna haja ya kuwekeza katika kilimo ili kukuza kipato cha kila mwananchi Ikungi"Twendeni tukajikite katika kilimo cha ufuta ili tukuze kipato chetu kwani Mkuu wa Mkoa Mhe Peter Serukamba ametoa agizo kwenye kila kijiji kuongezwa kwa maeneo ya kilimo"Amesema Mkuu wa Wilaya.Kwa upande wao uongozi wa Shanta Gold Mine wamesema wanashukuru serikali kuwapa ushirikiano wa karibu ili kuendeleza uwekezaji wao na hii misaada CSR wanatoa kwa moyo wote wakiamini mshikamano utaendelea kukua zaidi kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa