Halmashauri ya wilaya ya ikungi leo tarehe 24 mei 2024,imefanya kikao cha baraza la wafanyabiashara wa wilaya ya ikungi , Maafisa biashara ,TRA,NMB pamoja na wageni kutoka Baraza la Taifa biashara wakiambatana na mwakilishi wa TNBC .Katika Baraza hilo mgeni rasmi Mhe Thomas Apson mkuu wa Wilaya ya Ikungi amesema kuwa ili kuhakikisha biashara zinaenda vizuri lazima wafanya biashara na maafisa biashara wakutane au wakae pamoja ili kujadili changamoto zao na kujenga urafiki na watu wa TRA lengo uchumi wa nchi kupanda zaidi wanapofanya vizuri.Mwakilishi kutoka baraza la Taifa biashara Bi Sara ameongeza kwa kusema mabaraza haya ya wafanyabiashara na maafisa biashara pamoja TRA na mabanki ni muhimu sana kwani yanafuatiliwa mpaka ngazi za juu na Mhe Raisi Mama Samia Suluhu Hassani mwezi wa sita atafanya baraza la Taifa kuhusu wafanyabiashara na maafisa biashara wa nchi nzima .Mwenyekiti wa wafanya biashara ndg Kurwa nae ameomba mabanki wapunguze riba kwa wafanya biashara kutoka asilimia 20% au 24% mpaka 5% ili kumuendeleza zaidi mfanya biashara na TRA pia wampe nafasi mfanyabiashara kuangalia biashara yake kabla ya kudai leseni kwa yule anayeanza biashara .Pia Ndg Clement mfanya biashara ameomba fomu za kuombea mkopo zipunguze mlolongo wa taarifa haswa kwa wenyeviti wa vitongoji kwani wanadhalilika na kuwashauri maafisa biashara kutoa elimu maramara kwa wafanyabiashara ili wafanya biashara wasiwe wanakimbia wakiwaona maafisa biashara kwenye biashara zao Nae Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Diana amesema kuwa wafanyabiashara wanapoitwa kwenye mikutano wahakikishe wanaudhulia kwani kwenye vikao hivyo kuna elimu yenye faida kwao kuhusu leseni zaidi ya kufanyia biashara tu,pia ameongeza kwa kusema wafanya biashara wawe na upendo ,kusaidiana wao kwa wao na walipie leseni bila ya kusukumwa sukumwa.Mwisho mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ngd Haika Massawe amesema kuwa yote ameyapokea na kuahidi kufanyiwa kazi na kushauri TRA pamoja na Maafisa biashara kukaa pamoja kujadili mambo ya leseni na kuhusu biashara ya kiwango gani inafaa EFD machine.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa