Wilaya ya Ikungi yaadhimisha Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania kwa kujadili Mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabadiliko ya Kisiasa,Kijamii, kiuchumi na Kitamaduni Tanzania Tangu Uhuru hadi sasa na Mada hiyo ilitolewa na Mwalimu Adam Shule ya Msingi Elimu maalum Ikungi pamoja na Mada ya Hali halisi ya maadili na mabadiliko yake tangu Uhuru hadi sasa iliyowasilishwa na Bi Margaret Kapolesya Afisa Elimu msingi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.Hayo yamefanyika leo Tarehe 09 Disemba 2023 Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo Wazee,,Viongozi wa siasa,Viongozi wa Dini,Vijana,Watu wenye ulemavu na Watumishi wa Umma walishiriki Mijadala hiyo Baadhi ya maoni ya wananchi juu ya Mada hizo ni pamoja na kuishauri serikali kuanzisha makongamano ya mara kwa mara kujadili mambo yanayoihusu jamii inayowazunguka moja kwa moja ili kukuza uchumi,kupunguza Ukatili na mambo mengine mengi kuhusu maendeleo katika Wilaya ya Ikungi.Akisoma Taarifa katika Maadhimisho hayo Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Rashid M.Rashid amesema kuwa Wilaya ilipokea Maagizo kutoka Serikalini kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira na Kupamba hususani katika maeneo ya taasisi mbalimbali kufanya Bonanza la Michezo na katika Siku ya maadimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara kuwa na Mijadala mbalimbali na yote yametekelezwa kwa ubora unaostahili."Lengo ni kuimarisha jamii katika nyanja zote za kisiasa,kiutamaduni,kijamii na kiuchumi"Amesema Katibu Tawala.Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Mhe Mhe Thomas Apson akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba amesema kuwa ipo haja ya kukumbuka mambo waliyotuachia waasisi wetu na kuyaendeleza."Mwalimu Julias Kambarage Nyerere alisema tupambane na adui watatu na adui hao ni pamoja na Ujinga,Umasikini na Maradhi na kwa kiasi kikubwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu mpendwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anajitahidi kuhakikisha Elimu inapatikana kwenye Madarasa Bora,Vituo vya afya vinajengwa na Kutoa elimu mbalimbali juu ya maendeleo ya Jamii yetu".Amesesema DC ApsonMaadhimisho Haya yamebebwa na Kauli mbiu isemayo "Umoja na Mshikamano ni Chachu ya Maendeleo ya Taifa letu."
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa