Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo afungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo mashujaa wa Kilimo hasa vijana kutoka katika vijiji 87 Wilayani Ikungi.Akifungua mafunzo hayo leo Tarehe 15 Disemba 2023 Afisa Kilimo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaunganisha wakulima na watoa huduma za ugani katika ngazi zote kwa urahisi,kukuza kipato kwa wakulima kutokana na kilimo chenye tija, na kutafta masoko kwa uraisi ili kukuza uchumi wao.“Hivyo mafunzo haya yawe ni njia kuulekea uchumi mzuri kwa kila mkulima kwani wengi hulima maeneo makubwa bila kufata ushauri wa wataalamu na kujikuta wanapata mazao kidogo” Alizungumza Afisa KilimoMafunzo hayo yanatolewa na HEIFER Internatíonal ambayo ni NGO inayofadhili mradi wa FARMER VISIBILITY na unatekekezwa na kampuni ya DMA wakishirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo watagusia maswala ya huduma za ugani,faida za kutumia pembejeo bora za kilimo,kutafta masoko na kuyakuza ili wakulima kunufaika zaidi.Mara baada ya kufungua mafunzo hayo Afisa kilimo alikiri kupokea simu 87 aina ya FAMACO zenya thamani ya laki 3 kila moja zitakazotumiwa na vijana hao kuwakutanisha na wakulima katika vijiji vyao kupitia mfumo maalumu wa Farmpass.“Mjitahidi kuzitunza simu hizo ili ziweze kudumu zaidi na kubadili mfumo wetu wa kilimo kutokakwenye kulima kawaida hadi kulima kilimo chenye tija”Alisema Afisa kilimo.Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo afungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo mashujaa wa Kilimo hasa vijana kutoka katika vijiji 87 Wilayani Ikungi.Akifungua mafunzo hayo leo Tarehe 15 Disemba 2023 Afisa Kilimo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaunganisha wakulima na watoa huduma za ugani katika ngazi zote kwa urahisi,kukuza kipato kwa wakulima kutokana na kilimo chenye tija, na kutafta masoko kwa uraisi ili kukuza uchumi wao.“Hivyo mafunzo haya yawe ni njia kuulekea uchumi mzuri kwa kila mkulima kwani wengi hulima maeneo makubwa bila kufata ushauri wa wataalamu na kujikuta wanapata mazao kidogo” Alizungumza Afisa KilimoMafunzo hayo yanatolewa na HEIFER Internatíonal ambayo ni NGO inayofadhili mradi wa FARMER VISIBILITY na unatekekezwa na kampuni ya DMA wakishirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo watagusia maswala ya huduma za ugani,faida za kutumia pembejeo bora za kilimo,kutafta masoko na kuyakuza ili wakulima kunufaika zaidi.Mara baada ya kufungua mafunzo hayo Afisa kilimo alikiri kupokea simu 87 aina ya FAMACO zenya thamani ya laki 3 kila moja zitakazotumiwa na vijana hao kuwakutanisha na wakulima katika vijiji vyao kupitia mfumo maalumu wa Farmpass.“Mjitahidi kuzitunza simu hizo ili ziweze kudumu zaidi na kubadili mfumo wetu wa kilimo kutokakwenye kulima kawaida hadi kulima kilimo chenye tija”Alisema Afisa kilimo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa