Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewaagiza watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa -NHC- na Taasisi nyingine za Serikali kuhakikisha pindi wanapojenga majengo mbalimbali yakiwemo ya kibiashara au nyumba za makazi kutumia malighali zinazopatikana kwenye eneo husika ili kukuza uchumi wa wafanyabiashara na kukuza ajira kwa Watanzania.
Waziri Mkuu MAJALIWA ametoa maagizo hayo mjini Singida wakati akizindua jengo la uwekezaji la SINGIDANI lilijengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC ambao ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.4.
Uzinduzi wa jengo la kisasa la uwekezaji la SINGIDANI mjini Singida umewavutia wananchi wengi ambao wamefika katika eneo hilo kuja kushuhudia uzinduzi wake ambao umefanywa na Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA.
Katika hotuba yake ya uzinduzi wa jengo hilo, Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewaagiza watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC kuhakikisha wanatumia malighali za ujenzi wa majengo yanayopatikana katika eneo husika ili kusaidia kukuza uchumi wa wafanyabiasha na kuongeza ajira kwa wananchi.
Pamoja na Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA kusisitiza kuhusu utunzaji wa majengo yaliyojengwa lakini amesema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha idadi kubwa ya wananchi nchini wanapata makazi bora na kwa bei nafuu kupitia ujenzi unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa nchini.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI amesema ujenzi wa majengo ya biashara yanayojengwa na NHC hayatauzwa kwa wananchi bali yatakuwa yanapangishwa tu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa