Maafisa Elimu kata ,Wakuu wa Shule na Walimu Walezi (walimu wa nasihi) hapo juzi tarehe 17 mei ,2024 na jana wamepata mafunzo ya elimu ya stadi za maisha kutoka Wizara ya elimu,Tamisemi Na Shirika la CAMFED (Campagn For Female Education) kwa nia ya kusaidia Vijana na serikali kufika malengo.Katika Mafunzo hayo Mgeni rasmi Mhe Thomas Apson ameshukuru kwa ujio wa wawezeshaji hao kwani itasaidi Vijana kujikwamua na kutoka kwenye makundi ya maadili yasiyofaa na kupata ujuzi ambao utawasaidia Vijana maishani .Pia Wawezeshaji hao Bi Sekunda Mareshi,Bi Ruth Saibull na Patrick Mwalyepelo wameweza kuwaelimisha Maafisa elimu kata Wakuu na Walimu wa nasihi kwa kutoa elimu ya umuhimu wa mradi huo na lengo la kumbadilisha kijana .Waliongeza kwa kusema mradi huu utafanywa na Vijana walio tayari kujitolea kufundisha ambao wana elimu ya kidato cha nne na kuendelea .Mwisho wawezeshaji walisisistiza Maafisa ,wakuu na walezi kutoa matangazo ya maombi ya kazi hii kwa Vijana walio tayari kujitolea kufundisha.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa