Kamati Tendaji ya Tehama Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndg Justice Kijazi imefanya kikao kujadili uboreshaji wa mifumo mbalimbali inayotumika ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi.Mifumo hiyo ni pamoja na mfumo wa ukusanyaji wa mapato LGRCIS,Mfumo wa matumizi ya fedha za Halmashauri MUSE,mfumo wa kuandaa bajeti PLANREP,Mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa katika vituo vya kutolea Huduma za Afya FFARS,mfumo wa kutolea takwimu elimu sekondari na msingi BEMIS,Mfumo wa kusimamia mishahara ya watumishi HCMIS,Mfumo wa usajili wa wanafunzi elimu msingi PReM,Mfumo wa utunzaji taarifa za walengwa PSSN mfumo wa kutolea taarifa za wagonjwa GoT-HoMIS,Mfumo wa kutolea taarifa usimamizi wa shule SIS, na Mfumo wa vibali vya kusafiria.Pia kamati imeomba kuboreshwa kwa mtandao wa LAN,kuhakiki mara kwa mara mashine za kukushanyia mapato POS na kutoa elimu juu ya matumizi ya mashine hizo kwa watendaji,kuboreshwa kwa mfumo wa manunuzi TANePS lengo kuu la kuboreshwa mifumo hiyo ni kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato kama Halmashauri na kukuza maendeleo.Mwisho Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndg Justice Kijazi amepongeza juhudi za Afisa Tehama Bi Eva Myula kujitahidi kusimamia na kuboresha mifumo hiyo Halmashauri,Hospitali ya Wilaya,Shule na vituo baadhi vya Afya kuhakikisha mapato hayapotei na kusisitiza kufungwa kwa mifumo hiyo katika vituo vyote vilivyosalia pamoja na shule.MWISHOAfisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi14/09/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa