Katika maazimio ya kikao cha kawaida cha kamati ya Fedha na uongozi na Mipango, moja ya mambo yaliyopitishwa katika mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani la tarehe 28 hadi 29 Aprili 2021.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mh Ally Mwanga alisisitiza "migambo wote wanaofanya kazi kwa mazoea waondolewe ama wabadilishiwe mageti ili kupunguza mianya ya utoroshaji wa mapato unasababishwa namigambo wachache wenye tamaa"
Halmashauri ya Ikungi inategemea zaidi makusanyo ya ushuru wa minada na mazao kama chanzo kikuu chamapato ya ndani.
Imebainika baadhi ya migambo na baadhi ya watendaji wamekuwa sio waaminifu kwa kushirikiana na baadhi ya wafanya biashara kukwepesha ushuru.
Katika mkutao huo wa baraza la Waheshimiwa Madiwani pia walihimiza watendaji wa vijiji na kata kukusanya mapato, Kuruhusu ukarabati wa wa choo cha matundu sita na mfumo wa maji katika kituo cha afya ikungi. pia wajumbe walisisitiza kufanya taratibu za kupima maeneo yote yataasisi za serikali.
HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa