MWENGE wa Uhuru umeridhishwa na utekelezaji wa miradi mitano kwa sekta za elimu, maji, Barabara, utawala na maendeleo ya jamii-ambayo imegharimu takribani Shilingi Bilioni 1.4 zilizotolewa na serikali ndani ya Wilaya ya Ikungi mkoani hapa. Tarehe 13/08/2022
Miradi iliyopitiwa, kukaguliwa na hatimaye kuzinduliwa ni pamoja na mradi wa maji wa rafiki wa tenki kubwa na vituo vyake vya mtawanyo wa maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita zipatazo laki moja ambalo limejengwa na Kampuni ya Chakwale kwa kushirikiana na RUWASA mkoani hapa kwa fedha zaidi ya shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali kupitia mapambano dhidi ya Uviko 19.
Pia mwenge ulikagua na hatimaye kuridhishwa na ujenzi wa daraja la barabara ya Utaho-Makiungu lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja, mradi ambao unatekelezwa kwenye kijiji cha Minyinga kwa azma chanya ya kufungua fursa za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wakazi wa kata za Kituntu, Siuyu, Makiungu, Makotea na vijiji vingine jirani
Aidha, fedha takribani shilingi 700 milioni zilizotumika kwa mradi mwingine wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa halmashauri wilayani hapa ni kati ya miradi iliyoguswa na mwenge huo mwaka huu, utekelezaji ambao kukamilika kwake kunakwenda kupunguza umbali na uhaba wa malazi kwa watumishi na kuongeza ufanisi.
Zaidi, kiongozi wa ujumbe wa mbio za mwenge kwa mwaka huu, Nyanzabara Geraruma, kwa kushirikiana na wenzake Emmanuel Chacha, Rodrick Ndyamukama, Zadida Rashid, Grolia Peter na Ali Juma Ali walifurahishwa na kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ndani ya shule ya sekondari Issuna, mradi ambao umegharimu takribani shilingi milioni 41.
Pamoja na mambo mengine, mwenge wa uhuru kwa kauli mbiu ya ujumbe wa sensa kwa mwaka huu isemayo; “Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo: Shiriki kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo ya Taifa” uliridhishwa na hatimaye kuzindua mradi mwingine wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Rushwa kwa mlengo wa ustawi wa elimu wenye shabaha ya kuleta matokeo chanya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa