Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi pamoja na Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakaa meza moja na Mwekezaji kutoka Ujerumani Ndg Joachim Schtt Kutoka kampuni ya Qomahr wakishirikiana na Kampuni ya Techno Road ya Tanzania Bwana Erick Mome pamoja na Kijucha Makulago wanahitaji Hekta elfu 20 sawa na Ekari elfu 50 kwa ajili ya Kilimo cha umwagiliaji cha Alizeti na Kiwanda cha kukamua mafuta ya yakula.Wakizungumza katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Leo tarehe 08 Juni 2023 Mwekezaji anasema kuwa anatarajia kulima alizeti kwa ajili ya kukamua mafuta ya alizeti ghafi na kuuza ndani na nje ya nchi pia atalima alizeti kwa ajili ya mbegu za kisasa na kuwauzia wakulima mbalimbali Tanzania.Pia ameongeza na kusema kuwa kutakuwa na kilimo cha mkataba kwa wakulima wadogo wadogo ambao watalima kwa mbegu na pembejeo za kisasa na kumuuzia muwekezaji kwa ajili ya kukamua mafuta na kuyauza."Hii itapunguza uagizaji mafuta kutoka nchi zingine,ajira,kukuza teknolojia ya kilimo,na kuwafundisha watanzania kulima kisasa" alisema mwekezajiKwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji amewakaribisha wawekezaji na kuwaruhusu kutembelea maeneo watakayotamani kuwekeza wakiongozwa na Afisa Kilimo na kuwaomba wafate utaratibu watakaopewa na TIC ili kuipata ardhi hiyo na kuanza rasmi uwekezaji huo Wilayani Ikungi.Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi08/06/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa