Katika ziara ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi leo tarehe 15 Julai, 2024 katika Kata ya Misughaa kwenye mkutano na wananchi amepokea kero mbalimbali za wananchi wa Kata hiyo huku wakipongeza juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za kutosha ujenzi wa miradi mipya na umaliziaji wa miradi.
Kero hizo ni pamoja na upungufu wa majosho, ukosefu wa barabara inayounganisha Kata ya Misughaa na Kata ya Ntuntu, upungufu wa maji safi na salama katika Kata ya Misughaa pamoja na migogoro mbalimbali ya ardhi.Mkurugenzi amesema kuwa serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kila kero katika kata zote zinatatuliwa kwa wakati ili kupunguza na hatimaye kumaliza changamoto hizo.
Pia amewaomba wananchi kutunza msitu wa Mlili kwa manufaa yao kwani ni msitu ambao unapaswa kuingia kwenye mpango wa uzalishaji wa hewa ya ukaa itakayoingiza mapato makubwa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa manufaa ya Wilaya nzima hususani vijiji vinavyolizunguka eneo hilo.Aidha Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe ametoa Elimu juu ya umuhimu wa fedha za asilimia kumi za vijana, wanawake na watu wenye ulemavu zinavyoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali watakavyojiunga ili kuomba fedha hizo Halmashauri na kuanzisha miradi yao.
Pia Bi-Haika Massawe ni Mratibu wa uchaguzi wa serikali zamitaa Wilaya ya Ikungi amewasisitiza wananchi kujiandaa kikamilifu na chaguzi wa serikali za Mitaa mwaka huu kwa kujiandikisha katika daftari la kudimu la wapiga kura, kuwania ngazi za uongozi, pamoja na kupiga kura kwa viongozi watakao waongoza kuleta maendeleo katika vijiji vyao.
Kwa upande wake mwanasheria wa Wilaya ya Ikungi amewataka Wanachi kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazo waongoza katika utekelezaji wa majuku yao kadri wanavyokubaliana katika mikutano yao ya vijiji.@samia_suluhu_hassan@ikulu_mawasiliano@dr_philip_isdor_mpango
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa