Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi ameanza ziara ya siku tatu kutembelea Kata ya Misughaa, Kikio na badae kumalizia kata ya Ntuntu lengo ikiwa ni kusikiliza na kushughulikia kero mbalimbali za watumishi na wananchi katika Kata hizo.Ziara hiyo imeanza mapema hii leo tarehe 15 Julai, 2024 katika Kata ya Misughaa ambapo Mkurugenzi akiambatana na baadhi ya wakuu wa Idara na vitengo wamesikiliza kero za watumishi katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dkt Sheini ambapo kero kubwa imekua upungufu wa miundombinu wezeshi katika shule za msingi sekondari pamoja na vituo vya afya hali inayopelekea ugumu kwa watumishi kufanya shughuli zao za kila siku.
Akijibu maswali ya watumishi Mkurugenzi amesema tathimini ya ukarabati wa miundombinu yote katika Wilaya ya Ikungi ni zaidi ya bilioni 11 zinahitajika ambapo amesema Halmashuri itajitahidi kupunguza changamoto mbalimbali kadri fedha zitakavyopatikana.
Aidha amesema katika Kata ya Misughaa ametenga zaidi ya milinoni 80 kutatua kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na milioni 20 kumalizia ujenzi wa bweni la wanafunzi sekondari ya Dkt Sheni ambapo Mhe Waziri Nape alileta mifuko ya sumenti 400 kukamilisha bweni hilo, milioni 50 ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Sakaa lakini pia ameagiza kukamilishwa kwa vyoo zahanati ya Misughaa ili kupunguza adha iliyopo na kukarabati baadhi ya vyumba vya madarasa pamoja na kuhakikisha madawati yanatosheleza kwa wanafunzi.
Pia amepongeza juhudi za shule ya Sekondari Dkt sheini kutekeleza maagizo ya serikali juu ya wanafunzi kupata chakula wakiwa shule kwani wananchi wametekeleza kwa kiwango kikubwa na wanaakiba ya chakula cha kutosheleza mpaka mwaka 2025.Kwa upande wake Ndg Jonas Lutiga akimuwakilisha Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amesisitiza watumishi kufata maadili ya kiutumishi Kuanzia nidhamu mavazi na utekelezaji wa majukumu yao ya serikali ili kukuza maendeleo katika Kata ya Misughaa.@samia_suluhu_hassan @dr_philip_isdor_mpango @ikulu_mawasiliano @ortamisemi @ccmtanzania @tbctaifa @millardayo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa