Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Peter Joseph Serukamba amewataka wataalamu wa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuishi katika vituo vyao vya kazi ili kuhakikisha wanawafikia wakulima wengi kwa urahisi ili kutoa Elimu ya kilimo bora chenye tija kwa maendeleo ya Mkoa wetu.Hayo ameyasema leo alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo,Maafisa Kilimo,Maafisa Ugani na Madiwani Wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Halmashauri ambapo amewataka Wataalamu hao kuwahudumia kwa karibu wananchi ili waweze kupanda mbegu bora,kuzingatia matumizi ya Mbolea na kuongeza maeneo ya kulima ili kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na kuondokana na Umasikini."Nasisitiza haya nikiwa na maana natamani Mkoa wetu utajwe kuwa ni miongoni mwa mikoa inayotegemewa kwa kilimo cha zao fulani ambalo ni Alizeti ili kuipunguzia serikali mzigo wa kuagiza mafuta kutoka nchi za jirani."Amesema Mkuu wa Mkoa.Sambamba na hilo ameitaka Idara ya Kilimo kusimamia kwa karibu usambazaji wa mbegu za ruzuku kwa wananchi vijiji vyote kwa wakati na kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mbegu hizo iendene sambamba na uwekaji wa mbolea za kutosha kupandia na kukuzia lengo ni kupata mazao mengi katika eneo dogoAidha amemuagiza Mkurugenzi kufatilia utendaji kazi wa Wataalamu wa Kilimo kuwa wanaishi katika maeneo yao ya kazi,Kupima afya ya udogo na kutoa ripoti,Kasi ya uandikishaji wa wakulima, na Kushiriki kikamilifu ugawaji wa Mbegu za Ruzuku kwa Wakulima.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson Akishirikiana na Halmshauri amesema kuwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati na kusisitiza matumizi bora ya mbolea kwa wakulima kukuza sekta ya kilimo Ikungi na nchini kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa