• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Ikungi District Council
Ikungi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi ya Maadili
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Tekolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Utawala
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbailmbali
    • Fomu Malimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Vituo vya habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya picha
  • Takwimu za Wilaya
    • Sensa 2022
      • Matokeo ngazi ya Taifa na Mkoa
      • Matokeo ngazi ya wilaya na kata
      • Matokeo ngazi ya vijiji
      • Kasi ya ongezeko la watu
      • Idadi ya kaya
      • Idadi ya watu kwa umri
      • Matokeo ngazi ya tarafa
    • Takwimu za Elimu
      • Orodha ya Shule kwa kata
      • Idadi ya wanafunzi
        • Msingi
        • Sekondari
    • Nyanja ya Afya
      • Idadi ya vituo vya afya kwa kata
      • Afya nyinginezo
    • Ikungi yetu
    • Takwimu za miradi

MKUU WA WILAYA IKUNGI KUMRITHI TUNDU LISSU

Posted on: July 11th, 2019

Kwa hisani ya Nathaniel Limu-SINGIDA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Miraji Mtaturu ameshinda kura za maoni CCM kwa kupata kura 396 kati ya kura 634, kwa ajili ya kurithi kiti cha Ubunge cha aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ambaye alivuliwa Ubunge June 28, 2019. 


WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Singida Mashariki, wamepiga kura kupata mwana CCM mmoja ambaye atapeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 31.

Katika mkutano huo uliofanyika jana, wanachama 13 walichuana katika uchaguzi huo na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu, ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 396.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu kupoteza sifa.

Mbali ya Mtaturu, wana-CCM wengine waliochuana katika kura hizo za maoni ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni mstaafu Chiku Galawa aliyepata kura 40.

Wengine na kura zao katika nabano ni Thomasi Kitima (79), Martini Lissu (29), Lazaro Msaru (17), Hamisi Maulidi (12),  Mwanahamisi Mujori (7), Mariamu Nkumbi (7), Moris Mukhoty (4), Jeremia Ihonde (4), Sylivester Meda (3), Shilinde Kasure (1) na Emmanuel Hume (1).

Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa na utulivu, kila mgombea aliweza kunadi sera zake mbele ya wapigakura na kisha kuulizwa maswali kwa mujibu wa utaratibu uliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Katibu wa Sekreterieti CCM Taifa, Salum Leja.

Leja alisema kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wamekamilisha kazi yao ya hatua ya kwanza na sasa kinachofuata majina ya wagombea watatu yatakwenda katika vikao vya ngazi ya juu ya chama.

Akizungumza baada ya kutangazwa kushinda kura za maoni, Mtaturu, alisema kuwa Jimbo la Singida Mashariki limekuwa nyuma kimaendeleo, hivyo pindi atakapoteuliwa na chama chake anaomba ushirikiano na wananchi wote wa Singida Mashariki na Wilaya ya Ikungi kwa ujumla.

“Ninawashukuru wana CCM wenzangu kwa kunipa ushindi mnono na sote tunaona namna jimbo letu lilivyo nyuma kwa maendeleo, na pindi chama kikinipa ridhaa na kuwa mgombea, ninaomba wote tushirikiane ili tuweze kuleta maendeleo,” alisema Mtaturu,

Naye mshindi wa tatu katika kura hizo za maoni, Luteni mstaafu Chiku Galawa, alisema ameridhika na matokeo ya uchaguzi huo na atashirikiana na mwana CCM yeyote ambaye atateuliwa na chama kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo katika jimbo hilo.

“Sina kinyongo na nimeridhika kabisa na matokeo haya, kikubwa sasa tushirikiane kwa pamoja ili kuleta maendeleo,” alisema Galawa.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Ikungi, Noverty Kibaji alisema wanachama hao baada ya kupigiwa kura za maoni za ndani ya chama, walioshinda nafasi tatu za juu, majina yao yatawasilishwa vikao vya juu kwa uamuzi.

 “Uchaguzi huu umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za chama chetu na tunaamini vikao vya ngazi ya juu ndio vitakuwa na maamuzi nani atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi huu wa marudio,” alisema.

Matangazo

  • MPYA! MPYA! MPYA! TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPT 06, 2023 August 31, 2023
  • View All

Habari mpya

  • MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA YAZINDULIWA WILAYANI IKUNGI

    August 04, 2025
  • Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Awataka Vijana Kujishughulisha

    July 23, 2025
  • Pongezi Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Amali Samamba

    July 23, 2025
  • Ziara ya Ukaguzi wa Miradi Siku 10 Kabla ya Mwenge, RC Dendego Apongeza

    July 12, 2025
  • View All

Video

DC Muro atembelea Kata ya Mkiwa na kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mkiwa. Kazi inaendelea...
More Videos

Viunganishi vya haraka

Tovuti unganifu

  • EGA website
  • public service management
  • TAMISEMI website
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

    Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania

    Simu ya mezani: +255262964037/6

    Mobile:

    Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa