Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson mapema leo hii Tarehe 18 Disemba,2023 afungua mafunzo ya siku tano ya Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo kuhusu Uongozi kuanzia Tarehe 18 Disemba 2023 mpaka 22 Disemba 2023.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo Mhe Apson amesema kuwa mafunzo haya ni muhimu kwani yanaenda kuongeza uadilifu katika kazi na utawala bora wa watumishi na kwa wananchi pia."Ni mategemeo yangu kila mmoja wetu atashiriki kikamilifu Mafunzo haya ambayo yanatarajiwa kufanyika kwa siku tano yenye adhima ya kuimarisha utendaji wetu na hatimaye kuitumikia jamii inayotuzunguka kwa uadilifu mkubwa."Amezungumza Mhe DC ApsonMafunzo hayo yanafanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo Mwezeshaji Afisa Maadili Ndg Joshua Mwambande kutoka Sekretarieti ya Maadili Kanda ya Kati Dodoma amesema kuwa mafunzo haya yatagusa mada mbalimbali kama vile Maadili ya Viongozi wa Umma,Uwajibikaji wa Pamoja katika Sekta ya Umma,Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma,Utawala Bora,Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mengineyo mengi ambayo yatamsaidia kiongozi kuongoza eneo alilopo kwa ufanisi.Cha mwisho amewatakia viongozi na wananchi wote Heri ya Krismasi na Mwaka mpya huku wakisherekea kwa utulivu ili kuumaliza vyema mwaka 2023 hatimaye kuufikia mwaka wa 2024.MWISHOImetolewa na,Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi18/12/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa