Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ndugu Kastori Msigala akiwa pamoja na Wakuu wa Divisheni ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Ikungi leo Septemba 15, 2025 kwa kutembelea miradi inayotekelezwa katika Kata za Kikio na Misughaa.
Akiwa katika ziara hiyo, Msigala amesisitiza umuhimu wa matumizi ya mapato ya ndani ya Halmashauri katika kukamilisha miradi hiyo ili wananchi waanze kupata huduma stahiki mapema.
“Ni muhimu kutumia mapato ya ndani kumalizia miradi tuliyoianzisha ili wananchi waanze kupata huduma muhimu, mweka hazina chukua hilo kwa utekelezaji zaidi” amesema Msigala.
Aidha, ametoa wito kwa Idara ya Elimu Msingi, Manunuzi na Ujenzi kushirikiana kwa karibu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaohitajika.
Miradi ya Shule iliyotembelewa ni pamoja na ya Shule ya Msingi Sakaa, Msule, Munane, Simbikwa na Mankumbi pamoja na Shule ya Sekondari Dr. Shein.
Sambamba na hilo pia Miradi ya Afya iliyotembelea ni pamoja na maandalizi ya ujenzi katika Kituo cha Afya cha Misughaa, ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Msule na Matundu ya Vyoo.
Ziara hiyo inalenga kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi na kuimarisha usimamizi wa fedha za umma.
Hii ni miradi inayotekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2024/25 na 2025/26 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ili kurahisisha huduma kwa wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa