Mkuu wa Wilaya ya IKungi Ndg
Jerry Muro, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi pamoja na watendaji wa kata katika wilaya hiyo wamesaini mkataba wa lishe ili kuboresha afya katika wilaya hiyo...
Mkataba huo umesainiwa tarehe 02 Novemba, 2022 katika ukumbi wa Halmshauri ya wilaya Ikungi.
Awali kabla ya kusaini mkataba huo Mkuu wa wilaya alizungumza na watendaji na kuwasisitiza juu ya uwajibikaji ili kukuza maendeo ya wilaya hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi Kijazi amesema atawachukulia hatua kali watendaji wote wanaoenda kinyume na maagizo wanayopewa lengo ikiwa ni kuthibiti upotevu wa mapato katika kata mbalimbali zilizopo wilayani hapo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa