Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu Prof Joyce Ndalichako amekagua mafunzo ya vitalunyumba katika halmashauri ya Wilaya ya Ikungi…
Ukaguzi huo umefanyika tarehe 17 septemba,2022 na kuwapongeza vijana kwa juhudi na mafanikio waliyopata kwa kuhakikisha mazao yanakuwa bora kila wakati huku akimwomba mkandarasi kuwawekea miundombinu rafiki kwa utendajui wao wa kazi.“ katika kipindi cha mazao yaliyotoka mmewafunika kote nilikopita hongereni sana”alisema Ndalichako.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Jerry Murro pamoja na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mhe Richard Rwehumbiza walikuwa wenyeji katika wa msafara huo na kuishukuru serikali kwa kuiwezesha Wilaya ya Ikungi kuwa moja ya wanufaika wa mafunzo ya vitalunyumba ambavyo vinatengeneza ajira kwa vijana…
Pia Mhe Jerry Murro amesema kuwa katika kuongeza thamani juu ya ujenzi huo wa vitalunyumba, Wilaya ya Ikungi inapeleka mradi wa namna hiyo katika Tarafa nne jimbo la Singida Magharibi na Singida Mashariki ili kurahisisha mafunzo na hatimaye kunufaisha vijana wilayani hapo…
Kwa upande wao vijana wanaopata mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wameishukuru serikali na kuwashauri vijana wenzao kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji wa kisasa ili kujikwamua kiuchumi.
(Pichani ni Prof Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na wenyeji wake wakikagua mradi wa vitalunyumba halmashauri ya wilaya ya Ikungi)
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa