Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi aitikia wito mara baada ya wananchi wa kijiji cha Songandogo Wilaya ya Ikungi kumuhitaji kufanya nao mazungumzo mbalimbali yanayohusu maendeleo.Ziara hiyo ya Mkurugenzi imeanza mapema hii leo tarehe 19 Mei, 2024 katika kijiji hicho cha Songandogo kufanya nao mazungumzo ya maendeleo na kufanya mkutano wa ndani ambapo wananchi wameeleza mambo mbalimbali yaliyofanywa na serikali na utekelezaji wa miradi unaenda kwa Kasi Wilaya ya Ikungi.Aidha wameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miradi mingi kwenye kijiji chao na kusema mahitaji yao ni jengo la shule kumaliziwa kwa wakati kwani imekuwa kikwazo.Kijazi ameeleza na kusema anaitambua vyema changamoto hiyo na Halmashauri kwenye bajeti ijayo ameahidi kumalizia jengo hilo ili wanafunzi wasitembee umbali mrefu kutoka katika kaya zao"Nafurahi kwani mnatambua mchango mkubwa ambao serikali inatoa kwa wananchi wa Wilaya ya Ikungi hususani kijiji hiki, kwani mmekuwa kipaumbele kushirikiana kwa karibu na serikali kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa haraka hasa pale panapohitajika nguvu za wananchi" amezungumza Kijazi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa