Timu kutoka Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi imefika katika Kijiji Cha Matyuku kilichopo kata ya Kituntu kwa ajili ya kufanya tathimini ya madhara ya mvua . Maafa hayo yametokea usiku wa kuamkia tarehe 22 Januari, 2025 ambapo zaidi ya nyumba 13 zimeathiriwa na mvua hizo ambapo kaya tatu zimekosa makazi ya kuishi, baada ya mapaa ya nyumba zao kuezuliwa na mvua hiyo iliyodumu kwa zaidi ya masaa 6.
Diwani wa kata ya Kituntu Mheshimiwa Ally Ramadhani amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi pamoja na timu yake kufika katika kijiji cha Matyuku kufanya tathmini ya maafa haya na kuahidi kuwasaidia waathirika wa mvua hizo.
Ndugu Juma Msupha akimwakilisha Afisa Mipango wa wilaya ya Ikungi amesema " tumeshuhudia madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha , na tumeona nyumba 13 zilizopata madhara. Baada ya kukusanya taarifa hizi halmashauri itaona jinsi ya kuwasaidia waliopatwa na maafa haya"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa