Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson ametoa onyo kali kwa viongozi na wananchi wanaohusika na uvamizi wa msitu wa Mlilii na kuwataka kuacha mara moja kabla ya hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.
Akizungumza hii leo tarehe 07 Januari, 2025 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na kusema kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya itaanza operesheni maalum ya kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale waliohusika katika uvamizi huo wa misitu.
Aidha, DC amesisitiza kuwa serikali haitavumilia vitendo vya uharibifu wa mazingira na kwamba hatua kali zitachukuliwa ili kulinda rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Viongozi wa vijiji na kata pia wametakiwa kushirikiana na vyombo vya dola katika kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na uharibifu wa misitu ili kudhibiti uharibifu wa mazingira wilayani Ikungi.
Zaidi ya vijiji 26 katika Wilaya ya Ikungi vinatarajiwa kufaidika na Mradi wa Maendeleo wa Hewa ya Ukaa, ambao unatarajiwa kutekelezwa katika msitu uliopo kwenye pori la Kijiji cha Minyughe kata ya Makilwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa