Wanakamati wa Huduma za Uchumi Wapitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026
Wanakamati wa Huduma za Uchumi wamepitisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao kilichofanyika leo, tarehe 11 Februari 2025.
Makisio ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha yalijumuisha vitengo na divisheni mbalimbali. Kikao hicho kilijadili:
Aidha, vitengo vilivyojadiliwa vilihusisha:
Maswali kuhusu Maboresho ya Majosho
Wakati wa kikao, Mheshimiwa Omary Toto aliuliza kwa nini maboresho na ukarabati wa majosho unaingizwa kwenye bajeti wakati majosho hayo yanajiendesha.
Akijibu swali hilo, Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ndugu Issa Tweve, alisema:
"Fedha zinazopatikana kwenye majosho zinatumika kuyaendeleza kwa kununua madawa na kufanya ukarabati mdogo mdogo. Fedha zilizotengwa kwenye bajeti ni kwa ajili ya ukarabati mkubwa na uanzishwaji wa majosho mapya."
Ushauri wa Mwenyekiti wa Halmashauri
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mheshimiwa Petro Mtyama, aliishauri Halmashauri kutobana sana ukomo wa bajeti kwa divisheni na idara mbalimbali kupitia mapato ya ndani. Alisema kuwa hatua hiyo inasababisha shughuli nyingi kutokamilika kwa wakati au kutokufanyika kabisa.
Ushauri huo ulitolewa baada ya Ndugu Filbert Benedict kujibu swali lililoulizwa na Mheshimiwa Toto kuhusu kwa nini fedha zilizotengwa kwa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira ni kidogo na zinatolewa kidogo kidogo.
Ndugu Benedict alifafanua kuwa, kati ya shilingi milioni 24 (24,000,000) zilizotengwa kwenye bajeti inayoishia Desemba 2024, ni shilingi milioni 2.06 (2,060,000) pekee ndizo zilizotolewa kupitia mapato ya ndani.
MWISHO
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa